Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Utawala wa Ethiopia wakabiliwa na changamoto nyingi baada ya vita kuzuka Tigray

Ethiopia iko katika hali tete wiki hii. Hali katika nchi hiyo haieleweki baada ya baadhi ya miji muhimu kutekwa na waasi wa TPLF, na hivyo kufungulianjia kuelekea mji mkuu Addis Ababa.

TPLF iliongoza muungano tawala wa Ethiopia kwa takribani miaka 30 lakini ilipoteza udhibiti baada ya Abiy kuingia madarakani mwaka 2018 kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali.
TPLF iliongoza muungano tawala wa Ethiopia kwa takribani miaka 30 lakini ilipoteza udhibiti baada ya Abiy kuingia madarakani mwaka 2018 kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliapa Jumatano kuwazika maadui wa serikali yake na "damu yetu", wakati akiadhmisha kuanza kwa vita katika mkoa wa Tigray mwaka mmoja uliopita.

Waziri Mkuu huyo ambaye alishinda tuzo ya Nobel kwa kutatua mzozo wa muda mrefu na Eritrea, alisema "tutamzika adui yetu na damu yetu na mifupa na kuipandisha juu tena heshima ya Ethiopia."

Siku ya Jumanne Abiy Ahmed Jumanne alitangaza hali ya hatari na kisitisha baadhi ya shughuli na kutoa mamlaka yote kwa jeshi, huku utawala wake ukionekana kudorora. Hayo yanajiri wakati Alhamisi hii, Novemba 4, ni mwaka mmoja tangu vita kuanza.

Nani angefikiria mwaka mmoja uliopita kwamba Ethiopia ingekuwa hapa ilipo leo? Kilichoanza kama operesheni ya "kurejesha utawala wa sheria", kama serikali ya shirikisho ilivyobainisha, haraka ikabadilika na kuwa mauaji ya kimya kimya. Na sasa mji mkuu wa shirikisho, Addis Ababa, uko chini ya tishio la kutwaliwa na waasi wa TPLF na washirika wao wa Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) ambao wanampia vita Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Mshindi huyo wa tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019, alikuwa akizungumza siku moja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari nchini Ethiopia, na wakati vikosi vya Tigray vikitishia kusonga mbele kuelekea mji mkuu Addis Ababa.

TPLF iliongoza muungano tawala wa Ethiopia kwa takribani miaka 30 lakini ilipoteza udhibiti baada ya Abiy kuingia madarakani mwaka 2018 kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.