Pata taarifa kuu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Mgogoro Tigray wachochewa na 'ukatili uliokithiri'

Mgogoro katika Jimbo la Tigray umechochewa na "ukatili uliokithiri", ameshtumu leo Jumatano Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, akiwasilisha uchunguzi wa pamoja na Waithiopia, ambao unahitimisha na uwezekano wa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa katika jimbo hilo na pande zote.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alituma askari katika Jimbo la Tigray mwaka uliopita ili kuangamiza waasi wa TPLF.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alituma askari katika Jimbo la Tigray mwaka uliopita ili kuangamiza waasi wa TPLF. Yasuyoshi CHIBA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Ukiukwaji mkubwa na mashambulizi ambayo tumerekodi vinabainisha haja ya kuwakamata wahalifu, bila kujali kambi wanakotoka," amesema Michelle Bachelet mjini Geneva nchini Uswisi.

Hayo yanajiri wakati Washington imeichukulia vikwazo Ethiopia vya kutoingiza bidhaa zake kwenye soko la Marekani.

Ni katika barua kwa Braza la Wawakilishi, Congress, ambapo Joe Biden ameonya wabunge wa Marekani kuhusu nia yake ya kuziondoa Ethiopia, Guinea na Mali kwenye mkataba wa Agoa.

Nchini Ethiopia, ambako uasi wa Tigray umekandamizwa kwa kiasi kikubwa, rais wa Marekani amelaani ukiukaji wa kikatili wa haki za binadamu zinazotambulika kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.