Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Mapinduzi nchini Sudan: Jeshi laonya mashirika ya serikali dhidi ya maanamano

Nchini Sudan, tangu mapinduzi ya jeshi Jumatatu, Oktoba 25, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anakabiliwa na hasira ya mitaani. Lakini pia anapingwa na taasisi na watumishi wa umma ambao wametangaza kuutii mamlaka "halali".

Jeshi la Sudan limetumwa katika mji wa Khartoum tangu Jumatatu, Oktoba 25 kujaribu kuzima maandamano baada ya mapinduzi.
Jeshi la Sudan limetumwa katika mji wa Khartoum tangu Jumatatu, Oktoba 25 kujaribu kuzima maandamano baada ya mapinduzi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tayari mgawanyiko huu unaongoza diplomasia ya Sudan. Tangu Jumatatu, jeshi limekuwa likifanya msako katika mashirika ya umma makampuni ya serikali na kuwasimamisha kazi au kuwabadilisha wale wote wanaopinga mapinduzi hayo.

Takriban wanadiplomasia 70 wa Sudan wametangaza kutounga mkono mapinduzi ya jeshi. Baadhi walijiunga na mikutano ya waandamanaji iliyoandaliwa mbele ya balozi zao. Katika kulipiza kisasi, jeshi limewafuta kazi sita kati yao wakiwemo mabalozi mashuhuri nchini China, Uswisi, Ufaransa na Marekani. Baadhi, kama Balozi wa Umoja wa Mataifa huko Geneva, wamekataa: "kufukuzwa kazi kinyume cha sheria na kinyume na katiba".

Hatua ya kufutwa kazi yaripotiwa katika vyombo vya habari vya serikali

Wizara, vyombo vya habari vya umma na vyama vya wafanyakazi pia vimeingia katika upinzani dhidi ya mapinduzi hayo. Televisheni za serikali, redio na shirika la habari la taifa la Suna vilivamiwa na wanajeshi. Wakurugenzi wao walitimuliwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine wasio kuwa na chuki na jeshi. Hatu hii imeathiri sekta zote za umma. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Usafiri wa Anga pia amefukuzwa kwenye wadhifa wake.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alivunja vyama vyote vya wafanyakazi na vyama vya kitaaluma. Hadi mapinduzi ya mwaka 2019, vyama vyote vya wafanyakazi vilikuwa vikiongozwa na wafuasi wa serikali ya zamani. "Kurudi nyuma haiwezekani" ni mojawapo ya kauli mbiu zilizoenea sana mjini Khartoum tangu Jumatatu wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.