Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Mapinduzi Sudani:UNSC yapitisha azimio kwa kauli moja

Utawala wa kijeshi nchini Sudan ubnaendelea kutengwa kumataifa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kwa kauli moja kuhusu Sudan Alhamisi, Oktoba 28.

Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. POOL GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku kadhaa za majadiliano, Urusi na China hatimaye zimekubali kutia saini nakala iliyorekebishwa, kuelezea msimamo wa pamoja. Katika maandamano yanayoendelea kupinga mapinduzi ya kijeshi, mtu mooja aameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama.

Wakati maandamano ya watu wengi yakitarajiwa kufanyikasiku ya Jumamosi huko Khartoum na katika miji mingine kadhaa ya Sudan, ili kutaka raia kurejeshwa madarakani, diplomasia ya kimataifa imeanza kutumika wakati huu, dhidi ya mkuu wa jeshi Abdel.Fattah al-Burhan ambaye anaonekana kutengwa zaidi na ambaye amejikuta njia panda Alhamisi hii kwa sababu ya azimio hili liliopiprishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya kusitishwa kwa misaada ya kimataifa ya kifedha, baada ya kulaaniwa kwa maneno makali na Umoja wa Afrika, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka, katika mjadala mkali ambao awali ulizua mtafaruku lakini baadaye umepitishwa kwa kauli moja, kuanzishwa upya kwa "serikali ya mpito inayoongozwa na raia", likieleza" wasiwasi wake mkubwa juu ya jeshi kuchukuwa madaraka kwa nguvu”. Pia limelaani kamata kamat inayoendelea na kuvunjwa kwa taasisi za mpito nchini humo. Na kuomba "mazungumzo bila masharti" kutatua mgogoro uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi siku ya Jumatatu.

Tayari, siku moja kabla, balozi za nchi za Magharibi zilisema kuendelea kumtambua Abdallah Hamdok na baraza lake la mawaziri kama "viongozi wa kikatiba wa serikali ya mpito".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.