Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Mapinduzi Sudan: Umoja wa Afrika wasitisha Sudan kwenye taasisi zake

Baada ya mkutano mrefu, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeamua "kusitisha" Sudan kwenye taasisi za Umoja wa Afrika hadi serikali ya mpito inayoongozwa na raia irejee madarakani. Wakati huo huo, maafisa mbalimbali wa kiraia wanaendelea kusakwa na wengine tayari wamekamatwa.

Makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.
Makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. RFI/Miguel Martins
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake ya mwisho, iliyochapishwa Jumatano, Oktoba 27 asubuhi, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika "linalaani vikali" kitendo cha jeshi kufanya mapinduzi na kushikilia na "kupinga kabisa mabadiliko ya serikali kinyume na katiba". Baraza hilo limesema kitendo cha jeshi la Sudan "hakikubaliki".

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeomba rais wa Tume ya Umoja wa afrika kutuma mjumbe huko Khartoum kushiriki katika mazungumzo na viongozi wa kisiasa ili "kurejesha utaratibu wa kikatiba". Wakati huo ho Baraza hilo imekaribisha hatua ya viongzi wa mapinduzi ya kumuachiliwa huruWaziri Mkuu Abdallah Hamdok, lakini limetoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa, wakiwemo wajumbe wa serikali iliyopinduliwa.

Siku ya Jumanne jioni Abdallah Hamdok alirejeshwa nyumbani, lakini bado yuko chini ya ulinzi wa jeshi.

Nyumba yake iko Kafouri, eneo la kaskazini mashariki mwa Khartoum, kwenye kingo za Mto Blue Nile. Kulingana na vyanzo vya kijeshi, "hatua za usalama zimechukuliwa katika eneo hilo", ikimaanisha kwamba Waziri Mkuu aliyetimuliwa yuko chini ya kifungo cha nyumbani, ameripoti mwandishi wetu wa Khartoum, Eliott Brachet.

Abdallah Hamdok bado hana haki ya kuzungumza, lakini alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken Jumanne jioni. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatano hii, mabalozi wa Ulaya mjini Khartoum pamoja na mabalozi wa Uingereza na Marekani wanaomba kukutana na Abdallah Hamdok haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.