Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Maandamno yakita mizizi Sudan, kamata kamata yaendelea

Nchini Sudan, maafisa wa usalama wameendelea kukabiliana na waandamanaji baada ya jeshi kuchukua madaraka wiki hii, wakati huu rais wa Marekani Joe Biden akiongeza sauti yake kulaani kitendo hICho cha wanajeshi.

Maandamano yanatarajiwa kuendelea siku ya Ijumaa na wiki hii, waandamanaji wameendelea kufunga barabara kwa mawe na kuteketeza moto matairi kuonesha gadhabu zao.
Maandamano yanatarajiwa kuendelea siku ya Ijumaa na wiki hii, waandamanaji wameendelea kufunga barabara kwa mawe na kuteketeza moto matairi kuonesha gadhabu zao. © Marwan Ali/AP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, mwandamanaji mmoja aliuawa katika siku ya nne ya maandamano jijini Khartoum, kupinga hatua ya jeshi kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Watu wengine walijeruhiwa katika makabiliano hayo jijini Khartoum katika makabiliano makali ambayo jeshi linatumia mabomu ya machozi na risasi za mpira.

Rais wa Marekani Joe Biden na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linataka kurejeshwa kwa serikami ya kiraia haraka iwezekanvyo.

Aidha, Biden amelitaka Jeshi kuwaacha raia wa Sudan kuandamana kwa amani kudai kurejeshwa kwa serikali ya kiraia.

Benki ya Dunia, imesitisha utoaji wa fedha kwa Sudan, huku Umoja wa Afrika nao ukiisimamisha uanachama nchi hiyo kutokana na hatua ya jeshi.

Maandamano hayo yanatarajiwa kuendelea siku ya Ijumaa na wiki hii, waandamanaji wameendelea kufunga barabara kwa mawe na kuteketeza moto matairi kuonesha ghadhabu zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.