Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Waziri mkuu wa Sudan ajiunga na familia yake

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok hatimaye amerejeshwa nyumbani kufuatia shinikizo za Kimataifa, kufuatia kukamatwa na wanajeshi waliochukua madaraka nchini humo, huku vyama vya wafanyikazi vikiitisha mgomo wa kitaifa kulaani kinachotokea.

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok.
Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok. Ebrahim HAMID AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ofisi yake imethibitisha kurejeswa nyumbani kwa Hamdok lakini chini ya ulinzi mkali, licha ya Waziri wengine na viongozi wa serikali ya kiraia wanapoendelea kuzuiwa na jeshi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress alitaka Hamdok kuachiliwa haraka iwezekanvyo, huku Marekani ikisema itasitisha msaada kifedha kwa Sudan huku Umoja wa Ulaya ukitishia hatua hiyo baada ya jeshi kuchukua madaraka.

Siku ya Jumanne, Mkuu wa Jeshi nchini humo Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisema alikuwa amempa hifadhi Hamdok nyumbani kwake kwa sababu za kiusalama, na kuongeza kuwa jeshi lilichukua nchi ili kuepuka umwagaji damu.

Safari za ndege kuingia au kuondoka nchini humo zimesitishwa mpaka Oktoba 30, huku Mabalozi wa Sudan nchini Ubelgiji, Ufaransa na Uswizi, wakilaani mapinduzi hayo na kusema wanaendelea kuiheshimu serikali ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.