Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Maandamano yapamba moto kushinikiza jeshi kuachia madaraka Sudan

Mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan na kitendo cha jeshi kuwashikilia viongozi wa kiraia na kuvunjwa kwa taasisi za mpito yanasababisha wasiwasi mkubwa duniani kote.

Waandamanaji kusini mwa Khartoum baada ya mapinduzi, Jumatatu, Oktoba 25, 2021.
Waandamanaji kusini mwa Khartoum baada ya mapinduzi, Jumatatu, Oktoba 25, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mataifa mbalimbali duniani, yameelaani hatua ya jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu nchini Sudan na kumzuia Waziri Mkuu Abadalla Hamdok.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa "kuachiliwa mara moja" kwa Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, nayo Washington imetoa wito wa "kurejeshwa" kwa taasisi za mpito.

Marekani imelaani hatua hiyo ya jeshi na kutangaza kusitisha msaada wa Dola Milioni 700 kwa nchi hiyo.

Umoja wa nchi za Kiarabau na Umoja wa Afrika, umetaka mkataba wa kugawana madaraka kuheshimiwa na pande zote kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Awali, Mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fatttah al Burhan alitaka hali ya hatari na kuvunja serikali ya mpito.

Maandamano kupinga hatua ya Jeshi nchini humo yamekuwa yakiendelea usiku kucha katika jiji kuu Khartoum na ripoti zinasema wanajeshi wamewapiga risasi na kuwauwa waandamanaji watatu na mamia kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.