Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Maafisa wakuu kadhaa wakamatwa Sudan, uwezekano wa mapinduzi

Watu wasiojulikana wenye silaha wamewakamata viongozi kadhaa wa Sudan nyumbani kwao mapema Jumatatu hii, Oktoba 25, asubuhi baada ya mvutano wa wiki kadhaa kati ya jeshi na mamlaka ya raia katika nchi hii ya Afrika Mashariki. Abdalla Hamdok, waziri mkuu wa serikali ya mpito pamoja na maafisa kadhaa wa serikali wamekamatwa.

Siku ya Alhamisi, Oktoba 21, 2021, waandamanaji waliandamana katika mji mkuu wa Sudan na kote nchini kuunga mkono serikali ya kiraia ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, dhidi ya wanajeshi.
Siku ya Alhamisi, Oktoba 21, 2021, waandamanaji waliandamana katika mji mkuu wa Sudan na kote nchini kuunga mkono serikali ya kiraia ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, dhidi ya wanajeshi. © REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Habari za hivi punde kutoka Sudan zinasema kuwa Waziri Mkuu Abdallah Hamdok amekamatwa na kuzuia nyumbani kwake na wanajeshi.

Ripoti kutoka Khartoum zinasema, tukio hili limetokea, mapema siku ya Jumatatu kwa mujibu wa Televisheni ya nchi hiyo Al Hadath.

Aidha, inaelezwa kuwa, pamoja na Waziri Mkuu Hamdok, maafisa wengine wa serikali ya mpito  akiwemo Waziri wa Ulinnzi na Mawasiliano pia wamekamatwa.

Hii inakuja, kufuatia nchi hiyo kuendelea kushuhudiwa maandamano kati ya wanaoiunga mkono serikali ya mpito chini ya Hamdok na wale wanaotaka jeshi kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Serikali ya mpito inayoundwa kati ya raia na Baraza la kijeshi iliundwa mwaka 2019 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mlrefu Omar Al Bashir kufuatia maandamano ya wananchi, na ilipaswa kuongoza mpaka 2023 na kupisha Uchaguzi Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.