Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Mvutano Sudan: Wafuasi wa jeshi na wale wanaolipinga waingia mitaani Khartoum

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kuandamana jijini Khartoum, kundi moja likiunga mkono serikali ya mpito lakini lingine likishinikiza kujiuzulu kwa serikali hiyo.

Maandamano dhidi ya wanajeshi huko Khartoum, Sudan, Oktoba 21, 2021.
Maandamano dhidi ya wanajeshi huko Khartoum, Sudan, Oktoba 21, 2021. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yamepangwa na makundi pinzani, kwenye muungano wa vuguvugu la kiraia nchini humo FCC, ambao wamegawanyika kuhusu mwenendo wa serikali.

Vuguvugu la FCC lilikuwa katika mstari wa mbele kufanikisha maandamano ya mwaka 2019 yaliyomwondoa madarakani kiongozi wa zamani Omar al-Bashir.

Serikali hiyo ya mpito imeundwa kati ya jeshi na vuguguvu la FCC, lakini inaongozwa na Waziri Mkuu Abdallah Hamdok na inapswa kuongoza nchi hiyo hadi uchaguzi wa urais utakapofanyika mwaka 2023.

Kundi moja la vuguvugu hilo linamuunga mkono Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, huku kundi lingine likitaka jeshi kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Wakati wa maandamano hayo, viongozi wa pande hizo mbili, wametoa wito wa kila kundi kuandamana katika eneo lake na kutoshambuliana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.