Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Jeshi la Sudan ladai kumkamata waziri mkuu kwa ajili ya usalama wake

Baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, sintofahamu yaendelea kuripotiwa nchini Sudan. Jenerali wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan ameeleza sababu ya kukamatwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdallah Hamdok. Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ni mkuu wa jeshi na wa Baraza Kuu la Mpito ambaye alivunja, Jumanne, Oktoba 26, mamlaka ya mpito.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amefanya mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum, siku moja baada ya mapinduzi.
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amefanya mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum, siku moja baada ya mapinduzi. © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa hotuba yake, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amewalaumu raia kwa mapinduzi hayo, kutokana na mgawanyiko wao. Ameeleza kuwa migawanyiko ya kisiasa iliyotawala kipindi cha nyuma ilitishia usalama wa nchi. Wiki iliyopita kulishuhudia ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanajeshi, akiwemo waziri mmoja. Alishambulia kwa maneno sehemu ya Vikosi vya Kupigania Uhuru na Mabadiliko akivituhumu kutaka kutaifisha maamuzi ya nchi nzima dhidi ya chama cha siasa. Kulingana na Baraza Kuu la Mpito, siku zote wanatetea masilahi yao ya kisiasa badala ya maslahi ya nchi.

Kisha, akamtaja Waziri Mkuu wa zamani, Abdallah Hamdok: “Yuko nyumbani, nahangia naye chakula, tuko pamoja kila mara. Tulimtoa nyumbani kwake kwa ajili ya usalama wake. Amesema waandishi wa habari wanaweza kuanzia hivi sasa kwenda kumwona na kumuuliza maswali.

Kuhusu wafungwa wengine wa kisiasa, na miongoni mwao mawaziri watatu na maafisa kadhaa wa Vikosi vya Kupigania Uhuru na Mabadiliko, Abdel Fattah al-Burhan amesema kwamba watahojiwa na kwamba wale ambao miongoni mwao hawajakutwa na hatia yoyote watarejea nyumbani. Hata hivyo, wengine wanatuhumiwa kutishia usalama wa taifa.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amebaini kwamba anaunga mkono katibaya nchi, wakati hatua kadhaa za katiba hii zilisitishwa Jumatatu. Ameongeza kuwa Baraza Kuu sasa litaundwa na wajumbe wa kiraia kutoka majimbo tofauti ya Sudan pamoja na wanajeshi. Raia hawa watateuliwa baada ya majadiliano na maafisa wa kila jimbo.

Mabalozi wa Sudan walaani mapinduzi

Wakati huo huo, mabalozi wa Sudan nje ya nchi wameendelea kuonyesha msimamo wao. Baada ya balozi wa Washington, wawakilishi wa Sudan huko Paris, Brussels na Geneva wametia saini taarifa ya pamojaJumanne, Oktoba 26, "kulaani kwa maneno makali" hatua ya jeshi kuchukuwa madaraka kwa nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.