Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Viongozi wa Sudan wajaribu kutatua sintofahamu ya kisiasa inayoendelea

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, ameunda Kamati maalum kujaribu kutatua sintofahamu ya kisiasa na uchumi inayoshuhudiwa nchini humo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani Omar Al Bashir.

Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock
Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hamdok, ameunda Kamati hii baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri na miongoni mwa wanasiasa wanaounda Kamati hiyo ni kutoka upande wa upînzani.

Kiongozi huyo ametoa wito kwa makundi pinzani nchini humo kuchukuliana na kukumbatia mazungumzo ili kutatua mvutano wa kisiasa unaoshudiwa nchini humo.

Tangu tarehe 16 mwezi Oktoba, kumekuwa na maandamano jijini Khartoum, kushinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpito, inayoundwa na raia na wanajeshi.

Septemba tano, jaribio la kuipindua serikali hiyo halikufanikiwa, wakati huu uongozi wa jeshi unapotarajiwa kukabidhi uongozi wa baraza la serikali hiyo ya mpito kwa uongozi wa kiraia mwezi Oktoba.

Serikali ya mpito inatarajiwa kuongoza mpaka 2023, wakati uchaguzi utakapofanyika na kuundwa kwa serikali mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.