Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Mchakato wa mpito waingia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa

Jumatatu Oktoba 11, rais wa Baraza Kuu tawala, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametaka kufutwa kwa serikali. Kwa nadharia, hana madaraka hayo, jukumu hilo ni la Waziri Mkuu Abdalla Hamdok kuchukuwa uamuzi kama huo.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, rais wa Baraza Kuu tawala, ametaka kufutwa kwa serikali ya kiraia nchini Sudan.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, rais wa Baraza Kuu tawala, ametaka kufutwa kwa serikali ya kiraia nchini Sudan. SUDAN NEWS AGENCY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii inaendelea kuzidisha sintofahamu katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo, huku viongozi wa kiraia na kijeshi wanagawana madaraka wakiendelea kutupiana lawama.

Wiki tatu baada kutibuliwa kwa jaribio la mapinduzi, ambalo mamlaka inawahusisha wafuasi wa Omar al-Bashir, mchakato wa mpito wa Sudan umeingia katika mzozo wa kisiasa ambao haujawahi kutokea.

Tangu Septemba 21 na jaribio la mapinduzi lililoshindwa, jeshi lililokuwa madarakani limeongeza mashambulio dhidi ya serikali ya kiraia. Akiongea na umati wa wanajeshi siku ya Jumatatu, Jenerali al-Burhan alisema jeshi ndilo kikosi pekee cha kuaminika kinachoweza kulinda kipindi cha mpito nchini Sudan.

Kwa upande wao, viongozi wa kiraia wanaona jeshi kama linataka kuhujumu majaribio yoyote ya mageuzi. Wanatoa wito kwa marekebisho kamili ya vikosi vya usalama na wanashutumu majenerali kwa kutokuheshimu hati ya katiba iliyotiwa saini Agosti 2019.

Shida ni kwamba, vita hivi vya maneno vinajitokeza katikati mwa mgogoro katika eneo la mashariki mwa nchi. Katika Port Sudan, mamia ya waandamanaji kutoka kabila la Beja wamekuwa wakizuia vituo vya bandari kwa karibu mwezi mmoja. Shughulizi za Uagizaji na usafirishaji zimekwama,  hali ambayo inazidisha sintofahamu na uhaba wa mafuta wa bidhaa na mafuta kwa kila siku. Siku ya Jumatatu huko Khartoum, hakukuwa na mkate wowote katika maduka ya mikate kwa sababu akiba ya ngano ilikuwa imeisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.