Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Mshambulizi mapya ya anga yarindima Mekele, mzozo waongezeka

Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray, ulikumbwa na mashambulizi mapya yaliyoendeshwa na jeshi la anga la Ethiopia Jumatano, Oktoba 20, mashamblizi ambayo yalijeruhi watu wanane, kulingana na duru za hospitali.

Mekele, mji mkuu wa jimbo la Tigray, ullikubwa na shambulizi jipya la anga lililotekelezwa na jeshi la anga la serikali, Oktoba 20, 2021.
Mekele, mji mkuu wa jimbo la Tigray, ullikubwa na shambulizi jipya la anga lililotekelezwa na jeshi la anga la serikali, Oktoba 20, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, mashambulizi ya anga dhidi ya mnara wa mawasiliano yaliua watoto watatu na kujeruhi raia kadhaa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Habari kutoka kwenye uwanja wa mapigano bado ni ngumu kudhibitisha. Lakini inaonekana kwamba mapigano yamezidi tangu Oktoba 11 serikali ilipotangaza kuzindua mashambulizi makubwa dhidi ya waasi katika jimbo jirani la Amhara, ambapo kunaripotiwa mapigano makali.

Mlipuko mkubwa ulitikisa mji wa huo. Halafu, mara baada ya hapo, kulionekana moshi ukifumba kutoka ngome ya waasi. Kulingana na habari ya awali kutoka mji wa Mekele, eneo la viwanda nje kidogo ya jiji ndilo lililengwa na shambulio hilo.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, kwa upande wake, alikiri kwamba jeshi la serikali lilitekeleza shambulio hilo dhidi ya kiwanda kinachotumiwa na waasi wa Tigray. Kiwanda ambacho, kulingana na msemaji huyo, hutumiwa kwa mafunzo na kwa utengenezaji na ukarabati wa silaha kubwa. Waasi wamekanusha madai hayo, wakisema ni sehemu ya kutengeneza magari yaliyoharibika na ghala la matairi.

Kauli hizi zinazokinzana zinaonyesha awamu mpya ya mzozo. Mawasiliano yamekatwa tena, haiwezekani kujua kwa uhakika hali kwenye uwanja wa mapigano. Mapigano makali yanaripotwa karibu na miji ya Dessie na Kombolcha, njia muhimu ya kimkakati kwa kudhibiti jimbo la Amhara. Mwandishi wa habari kutoka Marekani amebaini kwamlba aliona misafara ya wanamgambo wanaokimbilia kuelekea mapigano, wakiwa wamejihami kwa mapanga. Kila upande unadai ushindi, ingawa hakuna hasara iliyotangazwa kwa upande wa raia.

Marekani imelaani "kuongezeka" kwa mapigano nchini Ethiopia. Msemaji wa wizara ya mabo ya nje ya Marekani Ned Price alisema kwenye Twitter Jumatano wiki hii: "Tumeona ripoti za kuaminika za mashambulio katika mji wa Mekele na viunga vyake. Marekani inalaani kuongezeka kwa vurugu, ambazo zinaweka raia katika hatari. Serikali ya Ethiopia na Chama maarufu cha Ukombozi wa Tigray wanatakiwa kumaliza vita na kuanza mazungumzo sasa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.