Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Serikali yakiri kutekeleza mashmbulizi ya anga katika mji wa Mekele

Angalau watatu wameuawa katika mashambulizi ya anga liliendeshwa na vikosi vya serikali kuu ya AEthiopia katika mji wa Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray.

Mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele, nchini Ethiopia, Januari 25, 2018.
Mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele, nchini Ethiopia, Januari 25, 2018. Wikimedia Commons Copyleft A. Savin
Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo limekuwa eneo linaendelea kukumbwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Abiy Ahmed na waasi wa Tigray kwa karibu mwaka mmoja. Wakati mapigano yameanza tena kwa nguvu ubwa tangu siku kumi zilizopita, serikali kwa mara ya kwanza ilitekelea mashambulizi ya anga katika mji wa  Mekele Jumatatu, Oktoba 18.

Angalau mashambulizi mawili ya angani yaliripotiwa Jumatatu asubuhi na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada na madaktari katika mji wa Mekele. Shambulio la kwanza,lililenga jkampuni ya saruji. YShambulio la pili, lililotekelezwa katikati mwa jiji, lililenga hoteli wakati mwingine inayotumiwa kama makao makuu na viongozi wa waasi wa Tigray wa TPLF.

"Huu ni uwongo kabisa"

Kwa upande wake, Addis Ababa imeelezea msimamo ake na kukanusha madai hayo. "Huu ni uwongo kabisa," alisema msemaji wa serikali kwanza. Halafu jioni, shirika la habari la serikali hatimaye lilitambua mashambulizi hayo, lakini likadai kuwa yalilenga miundombinu ya mawasiliano ya simu na sio raia.

Huko New York, Umoja wa Mataifa una wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa mpigano katinya vikosi vya serikali na waasi. Katibu mkuu wwa umoja huo, Antonio Guterres, alizitaja ripoti za mashambulio ya anga kuwa za kutisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.