Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Jeshi lazidua mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa Tigray

Maswali yameibuka kuhusu ikiwa kuna mashambulizi mapya ya kiwango cha juu kaskazini mwa Ethiopia? Mwishoni mwa wiki hii, vizuizi vingi vya magari ya kijeshi na makundi ya wanajeshi yameshuhudiwa karibu na jimbo la Tigray, ambalo limekuwa katika vita kwa mwaka mmoja sasa.

Wanajeshi wa Ethiopia wakipiga doria.
Wanajeshi wa Ethiopia wakipiga doria. PETER DELARUE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miezi mitatu baada ya eneo hilo kuchukuliwa na waasi wa Tigray, inaonekana kwamba serikali na washirika wake wanahamasisha vikosi vyao kupata udhibiti tena. Operesheni kuu za kijeshi zilitarajiwa mwishoni mwa msimu wa mvua nchini Ethiopia. Msimu ambao uko karibu kumalizika.

Na kama ilivyotangazwa, mapigano yakaanza tena. Vikosi vya jeshi vinaendesha mashambulizi ya angani kwa kutumia ndege zisizo kuwa na rubani vikisaidiwa na vikosi vya ardhini, kulingana na msemaji wa waasi wa TPLF. Kwa upande wake, serikali ilikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu operesheni za hivi karibuni.

Wasiwasi kwenye uwanja wa mapigano

Wanajeshi wa Tigray walivamia maeneo kadhaa katika eneo jirani la Amhara mwezi Julai mwaka huu, na inaonekana kuwa peresheni hii sasa inakusudia kukomboa miji hii. Lakini baada ya kushinda uchaguzi kwa muhula wa pili, Abiy Ahmed pia anaweza tena kudhibiti jimbo la Tigray na kuwasaka viongozi wake, kama alivyofanya mwezi Novemba mwaka jana. Kwa hili, aliajiri makumi ya maelfu ya wapiganaji katika miezi ya hivi karibuni na alipata ndege zisizo kuwa na rubani, hasa kutoka Uturuki, chanzo cha kidiplomasia kimebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.