Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Abraham Belay ateuliwa kuwa Waziri wa ulinzi wa Ethiopia

Waziri MKuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amemteua Abraham Belay  aliyekuwa kiongozi wa mpito katika jimbo la Tigray kuwa Waziri mpya wa Ulinzi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa uzinduzi wa muhula wake wa pili huko Addis Ababa Oktoba 4, 2021.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa uzinduzi wa muhula wake wa pili huko Addis Ababa Oktoba 4, 2021. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, kuapishwa siku ya Jumatatu, kuongoza taifa hilo la pembe ya Afrika kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Uteuzi wa Belay, ni miongoni mwa mabadiliko muhimu yaliyofanywa na kiongozi huyo mpya kwenye Baraza lake la Mawaziri 22 ambalo limeidhinishwa na wabunge.

Abraham Belay, anayetokea katika jimbo la Tigray aliongoza, jimbo hilo kuanzia mwezi Mei, wakati vikosi vya serikali vilivyokuwa vinapambana na waasi wa jimbo na kazi kubwa iliyo mbele yake ni kuhakikisha kuwa, eneo hilo linakuwa salama.

Aidha, Mawaziri watatu wameteuliwa kutoka vyama vya upinzani kwa kile ambacho Ofisi ya Waziri Mkuu imesema, inaonesha nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa serikali inamjumuisha kila mmoja.

Wizara ya Maji ambayo ilikuwa inaongozwa na Seleshi Bekele, katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo ipo kwenye mvutano wa matumizi ya maji ya Mto Nile kati yake na Misri na Sudan, sasa itaongozwa na Habtamu Itefa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.