Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Kufukuzwa kwa maafisa wa UN Ethiopia: Guterres ataka ushahidi wa "maandishi"

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameomba ushahidi wa maandishi kwa mashtaka ya kuingiliwa katika masuala yake ya ndani ambayo Addis Ababa imeshtumu maafisa saba wa Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Februari 11, 2020.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Februari 11, 2020. Getty Images via AFP - SPENCER PLATT
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii, Oktoba 6, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alighadhabishwa hasa wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ethiopia.

Kikako cha Jumatano kilikumbwa na mvutano katika majengo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alimuomba mwakilishi wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa nyaraka zinazothibitisha "tabia mbaya" na suala la "kuingiliwa" katika mambo yake ya ndani ambayo Addis Ababa inashtumu maafisa saba wa Umoja wa Mataifa, tuhuma zilizoilazimu Addis Ababa kuchukuwa uamuzi wa kufukuza nchini humo wiki iliyopita.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Antonio Guterres alikuwa amemuomba nyaraka hizi Waziri Mkuu wa Ethiopia ambaye alikuwa amezungumza naye. Walakini bado hajapokea chochote, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.