Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Ethiopia: Waziri Mkuu Abiy Ahmed atawazwa kwa muhula mpya wa miaka mitano

Jumatatu hii, Oktoba 4, Abiy Ahmed alianza muhula wa pili kama Waziri Mkuu wa Ethiopia. Mshindi rasmi wa uchaguzi wa wabunge wa mwezi Juni mwaka huu, Abiy Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019 anaanza kipindi kipya cha miaka katika uongozi wa Ethiopia, akikabiliwa na ukosoaji wa kimataifa kwa jinsi anavyoshughulikia mgogoro wa Tigray.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa kuapishwa kwake Oktoba 4, 2021 huko Addis Ababa.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa kuapishwa kwake Oktoba 4, 2021 huko Addis Ababa. REUTERS - TIKSA NEGERI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliapishwa mbele ya rais wa nchi hiyo, Sahle-Work Zewde, katika makao makuu ya Bunge Jumatatu hii asubuhi. Kwa hivyo Abiy Ahmed ameazimia kuanza kipindi kipya cha miaka mitano na anatarajiwa kutangaza serikali yake ndani ya wiki hiyo.

Baada ya sherehe ndogo katika makao makuu ya Bunge, waziri mkuu mpya alijielekeza katika eneo la Meskel, katikati ya mji mkuu wa Ethiopia. Hapa ndipo sherehe rasmi ya kutawazwa ilifanyika na ambapo Abiy Ahmed alihutubia taifa.

Kwa hafla hiyo, wakuu saba wa nchi za Afrika walmehudhuria sherehe hizo, ikiwani pamoja na marais wa Uganda, Kenya, Senegal na Nigeria.

Lakini mbali na sherehe hii, kutawazwa kwake kunakuja wakati muhimu. Kwa upande wa waziri mkuu, upande mmoja, yeye ndiye aliibuka mshindi katika ucaguzi ambao vyama vikuu vya upinzani vilisusia. Lakini pia kwa nchi hiyo, kwa sababu Ethiopia inahusika katika mzozo wa kidiplomasia juu ya vita vya Tigray. Addis Ababa iliwafukuza maafisa saba wa UN siku ya Jumapili na sasa inakabiliwa na vikwazo zaidi vya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.