Pata taarifa kuu
GUINEA

Guinea: Wakosoaji wakubwa wa Alpha Condé warejea nchini

Viongozi wakuu wanee wa upinzani na wakosoaji wakuu wa Alpha Condé ambao waliitoroka nchi hiyo baada ya kuhofia usalama wao wako nchini Tangu Jumamosi, Septemba 18 wakitokea uhamishoni.

Waandamanaji huko Conakry Septemba 18, 2021, wakishangilia kurudi kwa wapinzani wanne wa Alpha Condé, baada ya kukimbilia uhamishoni.
Waandamanaji huko Conakry Septemba 18, 2021, wakishangilia kurudi kwa wapinzani wanne wa Alpha Condé, baada ya kukimbilia uhamishoni. © AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Wapinzani hawa waku dhidi ya marekebisho ya katiba na kuwania kwa Alpha Condé kwa muhula wa tatu walikuwa wamekimbilia nje ya nchi.

Karibu wiki mbili baada ya mapinduzi, Ibrahima Diallo, Sékou Koundouno, mwanamuziki Djani Alfa na mwanablogu Fodé Sanikayi Kouyaté walilakiwa kama mashujaa na umati mkubwa wa watu huko Conakry.

Wapinzani hao wamleelezea furaha yao kuona wamerejea nchini na kusema kuwa bado vita vinaendelea kuhakikisha demokrasia inakita miziza nchini Guinea.

Walipongeza viongozi wa mapinduzi, hususan Kanali mamady Doumbouya kwa hatua waliochukuwa ya kupinga kule ambapo Alpha Condé alikuwa akiipeleka nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.