Pata taarifa kuu
GUINEA

UN yataka raia kurudi madarakani katika muda muafaka

Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Afrika Magharibi na Sahel Mahamat Saleh Annadif anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari uhusu ziara yake huko Conakry.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Afrika Magharibi na Sahel Mahamat Saleh Annadif anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari uhusu ziara yake huko Conakry. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Mahamat Saleh Annadif aliwasili Jumatatu huko Conakry. Alikutana viongozi wapya wa Guinea, mabalozi wanaowakilish nchi zao  nchini Guinea na viongozi wa vyama vikuu vya upinzani dhidi ya utawala wa rais wa zamani Alpha Condé.

Wote walipokea ujumbe sawa: "Tuliwatumia ujumbe rahisi, kusema tu kwamba tunataka kuwasikiliza, wana maoni gani juu ya mustakabali wa nchi yao, ni mabadiliko gani wanayotaka kwa nchi yao, ili tuweze kuongozana nao ili Guinea iweze kuondokana na hali inayoikabili kwa sasa ”.

Mwanadiplomasia huyo wa UN pia alikutana na rais huyo wa zamani wa Guinea bila kubaini walichokiongea. "Tulikutana na rais Alpha Condé, tuliomba usalama wake ulindwe vilivyo na apewe huduma zote za kimatibabu kwa kulinda afya yake. Na anaendelea vizuri ”.

Kwa muda wa kipindi cha mpito ambacho kinawatia wasiwasi raia wa Guinea, Mahamat Saleh Annadif alisema Umoja wa Mataifa haulazimishi. “Muda wa kipindi cha mpito utakuwa ule ambao Wraia wenyewe wa Guinea wataamua. Tunashauriana na ECOWAS na hadi sasa tumesema kuwa tunataka muda mzuri, lakini muda unaofaa unategemea raia wenyewe wa Guinea”.

Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Afrika huko Afrika Magharibi alionyesha wasiwasi wake juu ya kurudi kwa mapinduzi barani Afrika, hasa nchini Mali, Chad na sasa nchini Guinea, hali ambayo alisema inaweza kutelezwa kama " kurudi nyuma kwa kidemokrasia".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.