Pata taarifa kuu
GUINEA

Guinea: Hatima ya rais aliyeondolewa mamlakani Alpha Condé yajadiliwa

Kando na majadiliano ya kisiasa juu ya mustakabali wa Guinea, mazungumzo mengine yanaendelea, chini kwa chini, juu ya hatima ya Alpha Condé. Rais aliyeondolewa madarakani bado anashikiliwa na viongozi wa mapinduzi.

Rais wa Guinea aliyeondolewa madarakani, Alpha Conde.
Rais wa Guinea aliyeondolewa madarakani, Alpha Conde. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, uliweza kumuona mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini kwa sasa, Alpha Condé anakataa kuachia ngazi, yeye bado anadai kuwa ndiye rais wa Guinea.

Mamlaka ya kijeshi imewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Alpha Condé ambayo yeye kwa ukaidi anakataa kusaini. "Sijaoni akisaini karatasi hiyo," amesema mwanadiplomasia mmoja  kutoka jumuiya hiyo, ambaye ameongeza: "Anadhani bado ni rais". Mtazamo wa kisasa wa Alpha Condé ni kwamba, kulingana na chanzo kingine, aliomba ujumbe wa ECOWAS Ijumaa (Septemba 10) akitaka jumiya hiyo kumrudisha katika nafasi yake kama mkuu wa nchi.

EOWAS inapanga kukutana siku ya Alhamisi Septemba 16 katika mkutano utakaofanyika huko Accra, nchini Ghana ili kujadili ripoti ya ujumbe ulizuru Guinea sikuya Ijumaa ya wiki iliyopita. Ujumbe huo kwa mara nyingine ulitaka Alpha Condé aachiliwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.