Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Maandalizi ya mwisho kabla ya mashauriano ya kitaifa

Mashauriano ya kitaifa yanatarajiwa kuanza Jumanne, Septemba 14. Kwa wiki nzima, Kamati ya Taifa kwa ajili ya Maendeleo ya Guinea, CNRD, inaalika "wadau mbalimbali katika ujenzi wa taifa" kwenye mikutano katika makao makuu ya Bunge.

Bango lenye picha ya  Kanali Doumbouya, aliyeongoza mapinduzi Guinea, huko Conakry, Septemba 11, 2021.
Bango lenye picha ya Kanali Doumbouya, aliyeongoza mapinduzi Guinea, huko Conakry, Septemba 11, 2021. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mashauriano haya ya kitaifa, kazi bado inaonekana kuwa ngumu. Kuanzia Jumanne hii 10 asubuhi, vitaanza vikao vitakoa waleta wadau mbalimbali katika ujenzi wa taifa, na kila baada ya saa bili wadau mbalimbali watakutana kujadili mustakabali wa nchi yao.

Viongozi wa kisiasa ndio watakaofunguwa vikao hivyo, hata hivyo vyama vitakavyoshiriki mashauriano hayo havijatambuliwa. Lakini, wawakilishi wa vyama vyote wanaweza kuhudhuria vikao hivyo.

Kwa ujumla, mpango huu unakaribishwa na vyama hivi, "ambao utawezesha kukutana na viongozi wa mapinduzi", na "kuanza mazungumzo". Kuhusu chama cha RPG cha Rais Alpha Condé, maafisa wa chama hicho wanakutana kujadili iwapo watashiriki au la.

Jumanne hii, pamoja na vyama vya kisiasa, wawakilishi wa uratibu wa majimbo na viongozi wa dini wanatarajiwa. Siku ya Jumatano, itakuwa zamu ya mashirika ya kiraia, mabalozi, na mashirika ya raia wa Guinea wanaoishi nje ya nchi. Alhamisi, mashauriano yako wazi kwa wakuu wa kampuni za madini na mashirika ya waajiri. Mwishowe siku ya  Ijumaa, wa mwisho watakuwa mameneja wa benki na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.