Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Ujumbe wa ECOWAS kuzuru Guinea baada ya kutangaza vikwazo

Baada ya Guinea kufukuzwa katika Jumuiya ya ECOWS kutokana na mwenendo wake kufuatia mapinduzi ya kijeshi, ujumbe wa jumuiya hiyo unatarajia kuwasili leo Alhamisi nchini huko Conakry.

ECOWAS imesimamisha uanachama wa Guinea kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
ECOWAS imesimamisha uanachama wa Guinea kufuatia mapinduzi ya kijeshi. © NIPAH DENNIS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya ECOWAS katika mkutano wa dharura, saa 72 baada ya mapinduzi ambayo yalimuondoa mamlakani rais Alpha Condé huko Conakry; waliamua kuichukulia vikwazo Guinea Jumatano wiki hii.

Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mkutano uliofanywa kwa njia ya mtandao Jumatano. Kulingana na Reuters, uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Alpha Barry,aliyeshiriki kwenye mkutano huo wa viongozi wa nchi 15 za ECOWAS uliofanyika jana jioni kwa njia ya video, mjini Ouagadougou amesema Guinea kwa sasa imesimamishwa kwenye mabaraza yote ya kupitisha maamuzi ya jumuiya hiyo ya ECOWAS.

Vikwazo kwa kiwango cha chini, kwa sasa. ECOWAS "inapinga mabadiliko yoyote ya kisiasa kwa njia zisizo za kikatiba", na "inalaani vikali mapinduzi haya". Kwa hivyo Guinea imesimamishwa, lakini inaepuka hatua za kiuchumi, kama vile kusimamisha biashara au kufunga mipaka.Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS alisema kuwa mapinduzi ya kijeshi yalikiuka makubaliano ya jumuiya hiyo kuhusu utawala bora.

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso amefahamisha kwamba jumuiya hiyo sasa itauomba Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuidhinisha uamuzi wake huo. Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso amesema ujumbe wa upatanishi wa jumuiya hiyo utakwenda hii leo Alhamisi katika mji mkuu wa Guinea, Conakry kufanya mazungumzo na mamlaka mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.