Pata taarifa kuu
GUINEA

Mapinduzi Guinea: Jeshi lakabiliwa na shinikizo la kidiplomasia

Viongozi wa mapinduzi waliomtimua rais wa Guinea Alpha Condé mamlakani wanakabiliwa na shinikizo kali la kidiplomasia, baada ya kuwasili kwa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na kusimamishwa kwa nchi hiyo katika taasisi za Umoja wa Afrika (AU).

Ujumbe wa ECOWAS ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Conakry,  Septemba 10, 2021.
Ujumbe wa ECOWAS ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Conakry, Septemba 10, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS ililaani siku hiyo ya mapinduzi jaribio la mapinduzi lililoendeshwa siku ya Jumapili na mkuu wa vikosi maalum, Luteni-Kanali Mamady Doumbouya, dhidi ya Bwana Condé, 83, mkongwe wa siasa za Afrika Magharibi, ikidai aachiliwe na "kurejeshwa kwa katiba ya nchi" katika nchi hii masikini iliyojaa rasilimali za madini.

Ujumbe wa ECOWAS, ulioundwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi nne na mwenyekiti wa tume ya ECOWAS, Jean-Claude Kassi Brou, uliwasili Ijumaa asubuhi wiki hii katika uwanja wa ndege wa Conakry na ndege ya Jamhuri ya Ghana, ambayo ni mwenekiti wa Umoja wa Afrika.

Kuwasili kwa ujumbe huo kuliambatana na tangazo la Umoja wa Afrika la kuisimamisha Guinea katika taasisi za umoja huo.

Baraza la masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama ya AU imemtaka Mkuu wa Kamisheni ya umoja huo Moussa Faki kushirikiana na wadau katika kanda hilo juu ya mgogoro huo wa Guinea. Uamuzi huo wa Umoja wa Afrika umetolewa siku moja baada ya marais wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS kuchukua hatua kama hiyo. Lakini Waguinea wamezipokea hatua hizo kwa shingo upande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.