Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Wapinzani kadhaa waachiliwa

Kundi la kwanza la wapinzani kadhaa wa rais wa Guinea aliyeondolewa madarakani, Alpha Conde, waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la raia huko Conakry, wako huru tangu jana jioni.

Abdoulaye Diallo (katikati), meya wa zamani wa Kindia, baada ya kuachiliwa kutoka gereza kuu la Conakry Septemba 7, 2021.
Abdoulaye Diallo (katikati), meya wa zamani wa Kindia, baada ya kuachiliwa kutoka gereza kuu la Conakry Septemba 7, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa hao walio achiliwa huru ni pamoja na Abdoulaye Bah (UFDG), Etienne Soropogui (Valeurs Communes), Ismaël Conde, Kéamou Bogolan Haba (msemaji wa muungano wa Anad, unaojumuisha vyama zaidi ya hamsini vinavyomuunga mkono mwanasiasa wa upinzani Cellou Dalein Diallo), pamoja na Foniké Mengué, ambaye alikuwa Hospitali kwa matibabu.

"Tuko huru leo, uhuru hauan mpaka, ni kama kuzaliwa upya unapotoka gerezani. Ni furaha kuwa miongoni mwa familia yako, naamini kuwa hili lilikuwa jaribio maishani mwangu, na kwa hivyo sina chuki dhidi ya mtu yeyote, "Abdoulaye Bah ameiambia RFI.

Bogolan Keamou Haba ambaye ni msemaji wa muungano wa Anad, unaojumuisha vyama vya kisiasa zaidi ya hamsini, mashirika ya kiraia na yale yasiyo kuwa ya kiserikali ambayo yanayomuunga mkono kiongozi wa chama kikuu cha upinzani dhidi ya utawala wa rais wa zamani wa Alpha Condé. Yeye ni mmoja wa wafungwa wa kwanza kuachiliwa jana usiku.

Mimi ndiye mfungwa wa mwisho wa Alpha Condé, aliyekamatwa Julai 14 [...] Watu wa Guine walidai kwamba muhula wa tatu ubadilishwe na ni wazi muhula wa tatu umebadilishwa, ni ushindi ambao tumeshinda pamoja. Sasa kwa kuwa Alpha Condé ameenda, lazima tufungue mazungumzo haraka. Na tunaomba kila mtu akubali kuungana kwa sababu tunapaswa kulitumikia taifa.

Ismaël Condé, aliyefungwa na serikali iliyotimuliwa, anawapongeza viongozi wapya ambao anaomba kulitumikia taifa tofauti na mtangulizi wao. "Nina imani kwamba maafisa wa jeshi wamekuja na nia njema, tunataka kuwaamini kwa nia njema hii, kwamba kuondoka kwa utawala wa Alpha Conde hatimae ni enzi mpya kwa Guinea", amesema.

Imam wa Wanidara, El-hadj Abdoulaye Baldé, aliyefungwa jela tangu mwezi Oktoba 2020, anaelezea matakwa na kufanya sala na maombi kwa mafanikio ya mamlaka mpya: "Tunafurahi sana na jeshi la Guinea, tunafurahi sana na Kanali Mamadi Doumbouya na timu yake, tunamwomba Mungu awaonyeshe njia iliyo sawa. "

Viongozi wa mapinduzi nchini Guinea waliahidi kufanya kilio chini ya uwezo wao kuachiliwa haraka wanasiasa na wafuasi wa upinzani waliokamatwa chini ya utawala wa rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.