Pata taarifa kuu
GUINEA

Guinea: Ujumbe wa ECOWAS kuijadili hatima ya Alpha Conde

Ujumbe wa Cédéao hatimaye utawasili katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, Ijumaa Septemba 10, 2021. Ziara hii ni ya kutathmini hali halisi nchini Guine, siku tano baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Alpha Conde.

Alpha Condé akiwa katika kampeni ya uchaguzi huko Kissidougou, Forest Guinea, Oktoba 12, 2020
Alpha Condé akiwa katika kampeni ya uchaguzi huko Kissidougou, Forest Guinea, Oktoba 12, 2020 Carol Valadee/RFI
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi tayari imeonesha msimamo wake kuhusiana na hali nchini Guinea baada ya kukutana Jumatano wiki hii katika mkutano wa dharura. Imeisimamisha Guinea katika taasii zote za jumuiya hiyoiliomba kuachiliwa kwa rais Alpha Conde, ambaye anazuliwa kwa sasa  katika sehemu ya siri.

Ujumbe huu wa ECOWAS ulitarajiwa kuwasili jijini Conakry Alhamisi Septemba 9, na kuahirishwa hadi Ijumaa hii Septemba 10. Ujumbe huu unaundwa na na mawaziri kadhaa wa kigeni kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, ikiwa ni pamoja na Ghana, Togo Burkina Faso na Nigeria, pamoja na Rais wa Tume ya ECOWAS, Jean-Claude Kassi Brou.

Ujumbe Huu utakutana na viongozi wapaya wa CNRD, Kamati ya Taifa kwa ajili ya Maendeleo, inayoongozwa na Kanali Mamady Doumbouya na kutaka kufahamu nini nia ya kiongozi mpya wa Guinea. Ujumbe huo pia utataka kufahamu kuhusu hatima ya Alpha Condé, ambaye hajaonekana hadharani tangu picha yake kusambazwa Jumapili wakati alipokamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.