Pata taarifa kuu
GUINEA

ECOWAS kuijadili Guinea na kuichukulia vikwazo

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Arika Magharibi wanatarajia leo Jumatano kukutana ili kuijadili Guinea na kuna uwezekano wa kuichukulia vikwazo. Siku ya Jumapili, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ililaani mapinduzi ya jeshi na kukamatwa kwa rais Alpha Conde.

Watu wakishangilia pamoja na vikosi vya jeshi kwene mitaa ya Conakry, baada ya kukamatwa kwa rais wa Guinea Alpha Conde, wakati wa mapinduzi ya kijeshi, Septemba 5, 2021.
Watu wakishangilia pamoja na vikosi vya jeshi kwene mitaa ya Conakry, baada ya kukamatwa kwa rais wa Guinea Alpha Conde, wakati wa mapinduzi ya kijeshi, Septemba 5, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, ECOWAS ilidai kurejeshwa kwa Katiba ya nchi la sivyo Guinea kukabiliwa na vikwazo. Kufikia sasa kilichoombwa hakijafanyika na ni dhairi kwamba vikwazovitachukuliwa. Moja ya vikwazo hivyo ni kusimamishwa kwa muda kwa Guinea katika taasisi zote za ECOWAS. Mnamo Mei 30, Mali ilikabiliwa na vikwazo hivyo baada ya mapinduzi ya pili ya kijeshi katika kipindi cha miezi tisa.

"Hiki ni kiwango cha vikwazo" ambavyo vitajadiliwa Jumatano hii Septemba 8, amebaini waziri mmoja kutoka jumuiya hiyo ya kikanda. Je! Vikwazo hivyo vitakuwa vya kiwango gani na vya aina gani? Itakumbukwa kwamba mwaka jana, Mali ilikubwa na vikwazo vya kiuchumi hadi pale wanajeshi walikubali kuanza kipindi cha mpito cha miezi 18.

Katika mkutano huo wa dharura, viongozi wa Afrika Magharibi wanaweza pia kuteua mjumbe maalum au mpatanishi kuwasiliana na viongozi wa mapinduzi. "Kwa ujumla, tunaangalia kati ya marais wa zamani wanaoweza kupatikana," ameongeza waziri huyo. Miongoni mwa majina yanayopigiwa debe kuchukuwa nafasi hiyo ni Ernest Bai Koroma, rais wa zamani wa Sierra Leone.

Mara tu maamuzi yatakapoidhinishwa, Umoja wa Afrika utashikamana na ECOWAS na kutangaza vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Afrika unaweza pia kusimamisha Guinea katika taasisi zake, kama ilivyoifanya Mali mapema mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.