Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Mapinduzi ya kijeshi Guinea: Makabidhiano ya kwanza ya madaraka yafanyika

Katika hotuba ya dakika tano, kiongozi mkuu wa mapinduzi nchini Guinea, siku ya Kumatatu, aliahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayohusika na kuongoza mabadiliko ya kisiasa, lakini  muda haujatajwa.

Luteni-Kanali Mamady Doumbouya alipowasili kwenye makao makuu ya Bunge, Septemba 6, 2021.
Luteni-Kanali Mamady Doumbouya alipowasili kwenye makao makuu ya Bunge, Septemba 6, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Jeshi limeanza kuchukua nafasi ya mamlaka ya raia na sheria ya kutotoka nje usiku ilitangazwa kuanzia 4:00 usiku hadi saa 11:00 alfajiri. Wakati huo huo makabidhiano ya kwanza ya madaraka yalifanyika Jumatatu, Septemba 6, katika mikoa ya Kankan na Labé.

Huko Kankan, ngome ya Alpha Condé ambako Mamady Doumbouya anatoka, makabidhiano kati ya raia na wanajeshi yalifanyika Jumatatu wiki hii. Gavana na mkuu wa wilaya wamebadilishwa. Kulingana na mashahidi kutoka mkoa huo, shughuli zilisitishwa ka muda katika jiji la Haute-Guinée kabla ya kuanza tena kama kawaida baadae mchana.

Kiongozi wa shirika lakiraia katika mkoa wa Kankan, Louncény Chérif, ameelezea tukio lisilo kuwa la kawaida ambalo haikushabikiwa na watu wengi wala kupingwakwa viongozi wapya, "tofauti na wilaya zingine ambazo wanajeshi walilakiwa kwa vifijo na nderemo".

Amesema kuliripotiwa makundi madogo madogo ya watu, wakiongea kuhusu siasa na wengine, mbele  ya redio zao, wakifuatia hotuba ya Mamady Doumbouya iliyorushwa moja kwa moja kutoka makao makuu ya Bunge huko Conakry.

Huko Labé, katika eneo la Fouta Djalon, pia makabidhiano ya madaraka yalifanyika kati ya raia na wanajeshi. Lakini katika ngome hii ya chama cha UFDG, chama cha kiongozi wa pinzani Cellou Dalein Diallo, wakaazi walikusanyika mbele ya jengo ambako sherehe ilifanyika kuelezea kutoridhika kwao au hasira yao kwa gavana anayemaliza muda wake, kulingana na mashahidi kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.