Pata taarifa kuu
GUINEA

Mapinduzi ya kijeshi yanayojirudi Guinea, rais ashikiliwa na jeshi

Kamati ya Kitaifa ya kwa ajili ya Maendeleo inayoongozwa na mkuu wa vikosi maalum, Luteni-Kanali Mamady Doumbouya, imetangaza kumshikilia rais Alpha Condé na kusitisha Katiba ...tukio linalojirudia nchini Guinea.

Askari wa vikosi vya jeshi vya Guinea wakipiga doria katika kitongoji cha Kaloum huko Conkary, Septemba 5, 2021.
Askari wa vikosi vya jeshi vya Guinea wakipiga doria katika kitongoji cha Kaloum huko Conkary, Septemba 5, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Mapinduzi matatu ya kijeshi katika kipindi cha miaka sitini, majaribio ya mapinduzi kadhaa ya kweli au yanayodhaniwa, nchini Guinea jeshi limekuwa mwamuzi mkuu wa matukio hayo ya kisiasa na mabadiliko. Wakati wa utawala wa Sekou Touré, baba wa uhuru, majaribio ya kuhatairisha usalama wa nchi, mara kadhaa yalipangwa kutoka nje ya nchi yakimshinikiza rais kutoa uwezo mkubwa kwa jeshi katika usimamizi wa nchi.

Alipofariki dunia mnamo 1984, mrithi wake alichukua madaraka kupiti mapinduzi. Kisha kanali, Lansana Conté aakamtimua Louis Beavogui, rais wa mpito, na kuunda kamati ya jeshi ya kwa manufaa ya taifa. Mwaka mmoja baadaye, Kanali Diarra Traoré alijaribu bila mafanikio kufanya mapinduzi ya kijeshi, ambayo yalisababisha umwagaji damu katika jeshi.

Mnamo mwaka 1996, askari waliasi, Lansana Conté aliponea alinusurika kifo, lakini mwaka 2008 aliuawa, na siku moja baada ya kifo chake, Kepteni Moussa Dadis Camara alichukua madaraka kwa niaba ya Kamati ya Kitaifa ya Demokrasia na Maendeleo.

Kuingia madarakani kwa Alpha Condé, watu wengi wa Guinea walitarajia kuona demokrasia inakita mizizi, na mabadiliko kuwa ya amani. Lakini kuvunjwa kwa kikatiba na vile vile mapambano ya kisiasa yasiyo na ukomo na huruma yalizua sintofahamu na kuibuka kwa mgogoro wa kisiasa. Na bila kusema wazi, wanasasa  wengi nchini Guinea walitarajia kutokea kwa mapinduzi mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.