Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea : kiongozi wa mapinduzi Mamady Doumbouya aahidi serikali mpya

Siku moja baada ya jaribio la mapinduzi lililomuangusha mamlakani rais wa Guinea Alpha Condé, Luteni-Kanali Mamady Doumbouya amepokea mawaziri wa serikali ya zamani na wakuu wa taasisi mbalimbali Jumatatu hii Septemba 6. 

Wanajeshi wa vikosi vya jeshi vya Guinea washerehekea kukamatwa kwa rais wa Guinea Alpha Condé katika jaribio la mapinduzi huko Conakry Septemba 5, 2021.
Wanajeshi wa vikosi vya jeshi vya Guinea washerehekea kukamatwa kwa rais wa Guinea Alpha Condé katika jaribio la mapinduzi huko Conakry Septemba 5, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake, Luteni-Kanali Mamady Doumbouya ameahidi kuundwa kwa "serikali ya umoja wa kitaifa" na amehakikisha kwamba hakutakuwa na "kamata kamata" dhidi ya raia au viongozi wa serikali ya zamani au upinzani.

Mawaziri wa serikali iliyotimuliwa na maafisa kutoka majimbo mbalimbali waliitishwa na viongozi wa mapinduzi kwenda makao makuu ya Bunge kwa mkutano, huku wakitahadharishwa wale wote watakaopinga.

Mkutano huo ulirushwa nje ya Ikulu ya Watu juu ya spika. Alipowasili, kiongozi mkuu wa mapinduzi, Kanali Mamady Doumbouya amelakiwa na umati wa watu waliokuwa kwenye makao makuu ya Bunge. Sherehe ilianza kwa kukaa kimya dakika moja kuwakumbuka wahanga wa utawala wa Alpha Condé.

Kuundwa kwa serikali mpya

Viongozi wakuu wa serikali ya Alpha Condé wameitikia wito huo. Waziri Mkuu Ibrahima Kassory Fofana, Waziri wa Ulinzi Mohamed Diané, Waziri wa Usalama, msemaji wa serikali, Spika la Bunge la Amadou Damaro Camara na mkuu wa Mahakama ya Katiba wamehudhuria mkutano huo. Mawaziri wengine kadhaa pia walishiriki katika mkutano huo, kama vile mkuu wa Mamlaka Kuu ya Mawasiliano Boubacar Yassine Diallo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, CENI.

Baada ya kukutana kwa mazungumzo na vigogo wa serikali ya zamani, Luteni-Kanali Doumbouya alitoa hotuba ambayo aliahidi kuundwa kwa "serikali ya umoja wa kitaifa". "maafisa waandamizi katika wizara mbalimbali watahakikisha mwendelezo wa huduma hadi serikali mpya ijayo itakapotangazwa," amesema. Wakati huo huo, hati za kusafiri na gari za serikali lazima zikabidhiwe kwa mamlaka.

Kulingana na tangazo la msemaji wa jeshi kwenye runinga ya kitaifa leoJumatatu, mipaka ya ardhi na anga imefunguliwa tena kwa biashara na shughuli zingine za kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.