Pata taarifa kuu
GUINEA-UCHUMI

Guinea: Viongozi wa mapinduzi wajaribu kuwatoa hofu wawekezaji wa kigeni

Hali ya mambo imeanza kugeuka nchini Guinea baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua rais Alpha Condé Jumapili (Septemba 5). rais huyo bado yuko mikononi mwa kundi hilo la maafgisa wa jeshi na polisi waliofanya mapinduzi.

Luteni-Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi mkuu wa mapinduzi, anasalimu umati wa watu alipowasili kwenye makao makuu ya Bunge huko Conakry, Septemba 6, 2021.
Luteni-Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi mkuu wa mapinduzi, anasalimu umati wa watu alipowasili kwenye makao makuu ya Bunge huko Conakry, Septemba 6, 2021. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Alpha Condé, kiongozi wa nchi kwa zaidi ya miaka kumi, na mpinzani wa zamani wa kihistoria anaiacha nchi hiyo katika hali mbaya ya kiuchumi.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa tangu mapinduzi hayo ya kijeshi, Mamady Doumbouya alitoa wito kwa wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza nchini humo akisema kuwa halini shwari.

Hali ya kijamii na kisiasa na kiuchumi, "usimamizi mbovu wa kifedha, umaskini na ufisadi uliokithiri" ni miongoni mwa sababu zilizotangazwa na Luteni-Kanali Mamady Doumbouya kutetea mapinduzi yake ya kijeshi.

Mageuzi ya kiuchumi yaliyopitishwa na kukaribishwa na Benki ya Dunia wakati wa muhula wa pili wa Alpha Condé kwa kukuza ukuaji wa uchumi kwa hivyo hayatakuwa na wakati wa kuonyesha ufanisi wake au mipaka yake katika kuboresha maisha ya kila siku ya wananchi wa Guinea.

Na ili siku hizi za kwanza za mapinduzi ya kijesi zisizuie uchumi ambao bado unategemea uuzaji wa malighafi, kiongozi mkuu wa mapinduzi amejaribu kuwahakikishia washirika na wawekezaji wa kigeni, kwa kutangaza hadharani kwamba mikataba ya kiuchumi na mikataba ya madini iliyosainiwa chini utawala wa Alpha Condé itaheshimiwa.

Guinea ina akiba ya madini ya chuma, dhahabu na almasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.