Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Jumuiya ya kimataifa yalaani mapinduzi ya kijeshi Guinea

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Uchumi wa mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, na nchi mbalimbali inwa ni pamoja na Marekani na Ufaransa zimeshutumu na kulaani vikali mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea na kutaka Rais Conde kuachiliwa huru mara moja bila masharti.

Polisi ya Guinea, Jumapili hii, Septemba 5, 2021 huko Kaloum, Conakry wakati kuliripotiwa jaribio la mapinduzi.
Polisi ya Guinea, Jumapili hii, Septemba 5, 2021 huko Kaloum, Conakry wakati kuliripotiwa jaribio la mapinduzi. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Kanali Mamady Doumbouya, Mkuu wa vikosi maalum vya jeshi la Guinea, anayeongoza kundi lawanajeshi na maafisa wa vikosi vya usalama waliofanya mapinduzi, Jumapili mchana alitoa ujumbe kwenye redio ya taifa na kituo cha runinga cha RTG. Akizungukwa na wanajeshi wenye silaha, bendera ya Guinea begani mwake, alitangaza kuunda Kamati ya kitaifa kwa ajili ya Maendeleo ya Guinea, CNRD, na kuahidi mazungumzo yasiyobagua na yenye manufaa kwa minajili ya kuandaa katiba mpya.

Luteni -kanali Mamady Doumbouya, anasema jaribo la mapinduzililikuwa linahitajika Guinea kutokana na mvutano wa kisiasa uliyo kuwa ukiendelea.
Luteni -kanali Mamady Doumbouya, anasema jaribo la mapinduzililikuwa linahitajika Guinea kutokana na mvutano wa kisiasa uliyo kuwa ukiendelea. - MILITARY SOURCE/AFP

Awali waziri wa ulinzi alinukuliwa akisema jaribio la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa.

Hii inafuatia masaa mengi ya makabiliano ya risasi karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu, Conakry.

Guinea imekumbwa na mapinduzi matatu ya kijeshi katika kipindi cha miaka sitini.

Hatima ya Rais wa Guinea Alpha Condé haijulikani wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonyesha mikononi mwa wanajeshi, ambao walisema wamefanya mapinduzi.

Jeshi ambalo limedai kuchukua madaraka nchini humo limetangaza kwamba litafanya mkutano leo Jumatatu na mawaziri na wakuu wa taasisi zilizovunjwa jana mjini Conakry.

Mapinduzi hayo yanajiri baada ya kipindi kirefu cha mvutano wa kisiasa nchini Guinea. Mgogoro huo ulichochewa mwanzo na upinzani mkali dhidi ya hatua ya Rais Conde kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka uliopita.

Tangu wakati huo, Conde amekuwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa na hata kusababisha maandamano mitaani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.