Pata taarifa kuu

Ethiopi: Waziri mkuu Abiy asema wanauwezo kuajiri wanajeshi wapya milioni 1

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amesema Serikali yake inauwezo wa kuajiri wanajeshi wapya milioni 1, lakini akasema hatafanya hivyo ili kuheshimu muda wa usitishaji mapigano kaskazini mwa nchi hiyo kwenye eneo la Tigray.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshindi huyo wa tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019, ametoa matamshi haya ikiwa ni wiki moja imepita tangu mji wa Mekele uangukie tena mikononi mwa wapiganaji wa eneo hilo ambapo alitangaza Serikali kusitisha mapigano.

 

Wapiganaji wa Tigray, wamesema hatua ya kufanikiwa kuchukua mji wa Mekele na maeneo mengine ni ushindi kwao katika vita ya wale iliosema maadui zao.

 

Akizungumza mjini Addis Ababa, waziri mkuu Abiy Ahmed, amesema Serikali yake inaweza kuchukua muda wa wiki moja pekee kusajili wanajeshi wapya laki 1, ikiwa vikosi vya sasa vitaonekana havitoshi.

 

Maofisa wa karibu na waziri mkuu Ahmed, amesema uamuzi wa kusitisha mapigano ulichukuliwa ili kujipanga upya kuhusu namna ya kushughulikia mzozo wa nchi hiyo.

 

Viongozi wa eneo la Tigray, mwishoni mwa juma walijibu hatua ya utawala wa Addis Ababa, ambapo walisema mkataba huo wa usitishaji mapigano utaheshimiwa ikiwa vikosi vya Eritrea na vile vya kikanda vya Amhara vitaondoka kwenye mji huo.

 

Viongozi hao sasa wanataka jumuiya ya Kimataifa kuwawajibisha waziri mkuu Ahmed pamoja na rais wa Eritrea, Isias Afwerk, kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

 

Maelfu ya watu wameuawa tangu kuanza kwa vita kwenye eneo la Tigray mwishoni mwa mwaka jana, ambapo waziri mkuu Abiy Ahmed, aliagiza wanajeshi wake kuuchukua mji huo kutoka kwa aliowaita wasaliti wa nchi.

 

Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, watu zaidi ya laki 4 tayari wanakumbwa na njaa huku wengine zaidi ya milioni 1 na laki 8 wakielekea kukumbwa na baa la njaa.

Umeme na mawasiliano mengine kwenye mji huo yamekatwa huku safari za ndege kwenye mji huo nazo zikisitishwa.

Waziri mkuu Abiy Ahmed, pia amesisitiza kuwa Serikali yake itatoa kiasi cha dola za Marekani bilioni 2 ili kusaidia kuujenga upya mji wa Mekele na maeneo mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.