Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-TIGRAY

Watu 64 wauawa baada ya jeshi la Ethiopia kushambulia soko

Watu 64 wameuawa na wengine 180 wamejeruhiwa baada ya ndege ya jeshi la Ethiopia, kushambulia soko katika jimbo la Tigray Kaskazini mwa nchi hiyo.

Gari la jeshi nchini Ethiopia
Gari la jeshi nchini Ethiopia EDUARDO SOTERAS AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa kiongozi wa jimbo la Tigray Mulu Atsbaha, amesema shambulizi hilo lilolenga soko katika mji wa Togoga na mbali na idadi ya watu waliopoteza maisha kwa mujibu wa maafisa wa afya, idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa.

Jeshi la Ethiopia limekiri kutekeleza shambulizi hilo na kuongeza kuwa, lilikuwa linawalenga wapiganaji wa jimbo la Tigray.

Hata hivyo, walioponea shambulizi hilo, wamesema waliona mabomu kutoka angani yakiwalenga na kusababisha pia vofo vya watoto waliokuwa sokoni.

Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi hilo na kutaka uchunguzi wa kina kufanyika na tukio hili limetokea wakati huu wananchi wa taifa hilo wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.