Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Umoja wa mataifa wataka uchunguzi kuhusu shambulizi la anga kwenye jimbo la Tigray, Ethiopia.

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kufanyaka kwa uchunguzi kuhusiana na shambulizi la anga ambalo limeua idadi ya watu wasiojulikana, katika soko moja lenye shughuli nyingi, jimboni Tigray, nchini Ethiopia.

Lori lililoshambuliwa kwa bomu katika eneo la Mekele, mji mkuu wa Tigray, Ethiopia February 26 2021
Lori lililoshambuliwa kwa bomu katika eneo la Mekele, mji mkuu wa Tigray, Ethiopia February 26 2021 EDUARDO SOTERAS AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili limefanyika huku kukiwa na taarifa za waasi kudhibiti tena miji kadhaa nchini humo, huku kukiwa na tuhuma dhidi yao katika kuendeleza mauaji ya raia.

Msemaji wa jeshi la Ethiopia alisema Alhamisi hii kwamba shambulio hilo la angani kwenye soko katika eneo lenye vita la Tigray lililenga waasi, sio raia, huku akikanusha kuuawa kwa makumi ya watu wasio na hatia.

Kanali Getnet Adane amesema operesheni ya Jumanne katika mji wa Togoga ilikuwa yenye mafanikio ambapo wanajeshi watiifu kwa chama tawala waliopelekwa eneo hilo ni wenye ustadi mkubwa na kwamba waliweza kuwatofautisha waa wa eneo hilo la Tigray licha ya kuwa waasi hao walikuwa wenye kuvaa nguo za kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.