Pata taarifa kuu
SOMALIA

Hali ya utulivu yarejea Mogadishu baada ya wanajeshi waasi kurudi kambini

Wanajeshi wanaounga mkono upinzani walikuwa wameshilia ngome zao katika mji mkuu wa Somalia katika wiki za hivi karibuni wakipinga Rais Farmajo kuongezwa muda wa kusalia madarakani kwa miaka miwili.

Wanajeshi wa Somalia wamerudi katika ngome zao Ijumaa, Mei 7 baada ya makubaliano na waziri mkuu.
Wanajeshi wa Somalia wamerudi katika ngome zao Ijumaa, Mei 7 baada ya makubaliano na waziri mkuu. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Kuondoka kwao wenye ngome zao kunafuatia makubaliano yaliyofikiwa mapema wiki kati ya serikali na upinzani. Kwa kubadilishana kurudi kwenye kambi zao na kutoegemea upande kisiasa, hakuna vikwazo vitachukuliwa dhidi ya wanajeshi hao walioasi.

Mamia ya watu waliojihami kwa silahaza kivita waliondoka katika handaki walizochimba mwishoni mwa mwezi Aprili na kuondoa vizuizi vya barabarani ambavyo walikuwa wameweka. Halafu walijiunga na kambi nje ya mji mkuu siku ya Ijumaa, kisha kurudi kwenye kambi zao mahali pengine nchini.

Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe huko Mogadisico ambapo wengi bado wanakumbukumbu ya yaleyaliyotokea Aprili 25, wakati kulizuka makabiliano kati ya vikosi vya serikali na vile vinavyounga mkono upinzani, kufuatia kuongezwa muda wa Rais Farmajokusalia madarakani kwa miaka miwili. Siku hiyo, kati ya watu 60,000 na 100,000 walitoroka makazi yao kufuatia vurugu hizo, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.