Pata taarifa kuu
SOMALIA

Somalia yatoa wito kwa raia wake waliokimbia kurejea

Serikali ya Somalia imewataka raia wake waliokuwa wamekimbia makwao kwa hofu ya usalama, warejee nyumbani baada ya hali ya utulivu kurejea.

Somalia yatoa wito kwa raia wake waliokimbia kwa hofu ya usalama wao kurejea nyumbani.
Somalia yatoa wito kwa raia wake waliokimbia kwa hofu ya usalama wao kurejea nyumbani. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Mohammed Farmajo, akithibitisha kurejea hali ya utulivu kwenye jiji kuu la Mogadishu, amesema anapanga kuwasilisha hoja bungeni kuidhinisha Uchaguzi Mkuu kufanyika, hili likijiri baada yake  kusaini awali, sheria  ya kuongeza utawala wake kwa miaka miwili.

Waziri mkuu  Mohamed Hussein Roble, kwa upande wake amewataka raia wa nchi hiyo waliokuwa wametoroka kufuatia mapigano mwishoni mwa wiki iliyopita,k urejea nyumbani na kwenye biashara zao, akisema wanajeshi watawapa usalama wakati wanarudi.

Roble licha ya kuwa mshirika wa rais Farmajo ni miongoni mwa viongozi waliotangaza wazi kutofautiana na rais kuendelea kutawala kwa miaka miwili zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.