Pata taarifa kuu
SOMALIA

Rais wa Somalia asalimu amri, akubali kutoongeza muhula wake

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ametoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi nchini humo na kurejelewa tena kwa mazungumzo ya kisiasa wakati huu nchi hiyo inapoanza kushuhudia vurugu za kisiasa baada ya bunge nchini humo kumwongezea muda wa miaka miwli kuendelea kuwa madarakani.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama  Farmajo.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama Farmajo. Riccardo Savi / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya rais Mohamed Abdullahi Mohamed inapingwa na wanasiasa wa upinzani na jumuiya ya kimataifa. Machafuko yanatishia usalama wa nchi hiyo.

Rais Abdullahi Mohammed wa Somalia amesema ataliondosha jaribio la kuongeza muhula wake kwa kipindi cha miaka miwili, kutokana na kile kinachoonekana kama shinikizo la ndani na nje ya taifa hilo.

Kwa sasa Rais Abdullah anaonesha kuwa tayari na kuendelea na uchaguzi, wenye kujikita katika makubaliano ya Septemba 17, ambayo yalihusisha serikali yake na viongozi wa majimbo ambao umekuwa ukisisitizwa na jumuiya ya kimataifa.

Naye Waziri Mkuu Mohammed Hussein Roble, amevitolea wito vikosi vya usalama kurejea makambini. Na kutaka Somalia irejee katika meza ya mazungumzo, huku akiwataka pia viongozi wa kisiasa kuacha vitendo vyoyote ambavyo vinaweza kuathiri hali ya usalama wa taifa hilo kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.