Pata taarifa kuu
SOMALIA

Somalia: Rais Farmajo afuta hatua ya kuongezwa muhula wake

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, kwa jina maarufu Farmajo, amelihutubia Bunge leo Jumamosi (Mei 1) wakati nchi hiyo ikiendelea kukumbwa na mvutano mkubwa.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo huko Mogadishu, mara tu baada ya kuchaguliwa kwake,  Februari 8, 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo huko Mogadishu, mara tu baada ya kuchaguliwa kwake, Februari 8, 2017. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Ametangaza kuwa ameachana na nia ya kusalia madarakani kwa kipindi cha miaka miwili baada ya Bunge kupitisha mswadawa sheria unaoongeza miaka miaka miwili kwa rais kuendelea kusalia mamlakani.

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ametoa wito wa kuanza tena kwa mazungumzo. Hotuba yake imekwa ikisubiriwa kwa hamu

Katika uamuzi ulioonekana kuwa ni kinyume cha katiba, Baraza la Bunge  lilipiga kura kuongeza miaka miwili kwa muhula wa rais kusalia madarakani.

Shinikizo limeongezeka katika siku za hivi karibuni kutoka pande zote kwa Bunge kufuta kuongezwa kwa muhula wa urais na kuwezesha kuanza tena kwa mazungumzo. Tena Ijumaa jioni, maandamano yanayounga mkono upinzani yalizuka katika mji mkuu, Mogadishu.

Bunge latakiwa kurejelea uamuzi wake

Akiongea mbele ya wabunge katika makao makuu ya Bunge, amewataka wabadilishe uamuzi wao kuongezwa kwa muhula wake wa kipindi cha miaka miwili na kuruhusu kurudi kwenye meza ya mazunumzo na makubaliano ya Septemba 17 mwaka uliyopita.

Makubaliano haya, yaliyosainiwa kati ya serikali na serikali za shirikisho, yalikuwa yaliruhusu uchaguzi ufanyike kabla ya kumalizika kwa muhula wa rais Farmajo mnamo Februari 8. Walakini, kutokubaliana kati ya vyama tofauti juu ya maandalizi ya kura kulizuia mchakato wa uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.