Pata taarifa kuu
SOMALIA

Umoja wa Afrika wamkosoa rais wa Somalia kwa kujiongezea muhula wake

Muhula wa Mohamed Farmajo, ambao ulimalizika mwezi Februari, umeongezwa kwa miaka miwili. Uamuzi huo uliibua ghasia na "ulilaaniwa" Alhamisi (Aprili 22) na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, ambalo litatuma mjumbe maalum kujaribu kuiondoa nchi hiyo kwenye mgogoro huo.

Le président de la Somalie, Mohamed Abdullahi Mohamed «Farmajo», le 26 novembre 2018.
Le président de la Somalie, Mohamed Abdullahi Mohamed «Farmajo», le 26 novembre 2018. Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati nchi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa na uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka jana bado haujafanyika, bunge nchini Somalia lilimruhusu rais wa nchi hiyo kusalia madarakani kwa miaka miwili zaidi, Ingawa muhula wake ulimalizika mwezi waFebruari.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Mataifa linabaini kwamba kuongezwa kwa muhula wa Mohamed Farmajo "kunaharibu umoja na utulivu wa Somalia" wakati "hatua ya upande mmoja wa bunge" inatishia "amani na usalama".

Kwa upande wa taasisi hii ya Umoja wa Afrika, makubaliano ya uchaguzi wa Septemba bado ni "chaguo bora zaidi kuelekea uchaguzi wa kuaminika". Imeomba mjumbe maalum kutumwa mara moja huko Mogadishu.

Marekani, Uingereza na Jumuiya ya kiuchumi na maendeleo ya nchi za afrika Mashariki (IGAD) wamekaribisha taarifa hii, inayokosoa uamuzi wa Mohamed Farmajo na bunge la nchi hiyo, wakati rais huyo amerudi kutoka Kongo Kinshasa ambapo alimuomba rais Felix Tshisekedi, ambaye ni rais wa sasa waUmoja wa Afrika, AU, kupatanisha pande zinazokinzana nchini Somalia.

Hali hiyo inasababisha mvutano wa kikanda. Mogadishu inashutumu Kenya na Djibouti kwa kujaribu kushawishi PSC na kukiuka uhuru wa Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.