Pata taarifa kuu
NIGERIA

Nigeria: Watu watoroka mji wa Damasak kufUatia mashambulizi ya wanajihadi

Jeshi la Nigeria linadai kuwa limeudhibiti tena mji wa Damasak, ulioko kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno, baada ya mashambulio kadhaa ya umwagaji damu yaliyofanywa na kundi la Boko Haram. Angalau watu 18 wameuawa, viongozi wamesema. Watu wanatoroka eneo hilo.

Askari wa Nigeria akitoa ulinzi karibu na Mto Yobe kaskazini mashariki mwa Nigeria (picha ya kumbukumbu).
Askari wa Nigeria akitoa ulinzi karibu na Mto Yobe kaskazini mashariki mwa Nigeria (picha ya kumbukumbu). Florian PLAUCHEUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mji huo, ulio karibu na mpaka na Niger, umendelea kukumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la ISWAP - kundi lililojitenga na Boko Haram na kujiunga na Islamic State. Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu wameendelea kulengwa katika mashambulizi hayo na watu wametoroka makaazi yao kuelekea Maiduguri au Diffa, mpakani.

Maelfu ya watu walio katika mazingira magumu walivuka Mto Yobe ambao unatenganisha Nigeria na Niger katika siku za hivi karibuni, katika jaribio la kutoroka mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram - kulingana na mashirika yasio ya kiserikali. Wengine walielekea Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, ambapo zaidi ya watu milioni moja tayari wamekimbia vitisho vya wanajihadi.

Wakazi 85,000 wa mji wa Damasak wamekuwa wakitegemea sana misaada ya kibinadamu. Lakini mashirika ya kutoa misaada yalizimika kuondoka katika mji huo wiki moja iliyopita lililopita.

Shambulio la kwanza dhidi ya mji huu unaopakana na Ziwa Chad lilitokea Jumamosi Aprili 10 na kulenga moja kwa moja ofisi za Umoja wa Mataifa na mashrika yasio ya kiserikali katika mji huo. Washambuliaji hao pia waliiba vifaa mbalimbali katika hospitali, ikiwa ni pamoja na gari la wagonjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.