Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Malawi: Matokeo ya kwanza kuanza kutangazwa Alhamisi

Raia wa Malawi wanaendelea kusuburi  matokeo ya marudio ya uchaguzi wa urais uliofanyika jana Alhamisi kufuatia agizo la mahakama ya kikatiba mwezi Februari.

Rais wa Malawi Peter Mutharika alipiga kura katika uchaguzi wa rais wa Juni 23, 2020 huko Thyolo.
Rais wa Malawi Peter Mutharika alipiga kura katika uchaguzi wa rais wa Juni 23, 2020 huko Thyolo. REUTERS/Ernest Mwale
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya katiba hapo Februari 3 iliamuru kuwa uchaguzi huo urudiwe, ikiamua kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwanzo yamebatilishwa kwa sababu ya ushahidi mkubwa wa mapungufu pamoja na kughushi kura katika uchaguzi uliofanyika Mei 2019.

Katika uchaguzi huo wa mwezi Mei mwaka 2019, Mutharika alitangazwa kuwa mshindi akiwa na asilimia 38 ya kura zote zilizopigwa, Lazarus Chakwera alikuwa wa pili na asilimia 35 naye aliyekuwa wakati mmoja makamu wa rais Saulos Chilima akiwa wa tatu na asilimia 20 ya kura zilizopigwa.

Chakwera na Chilima waliwasilisha kesi dhidi ya uchaguzi wa Mutharika na kuongoza maandamano ya kutaka maafisa wa tume ya uchaguzi nchini humo kujiuzulu.

Katika kesi yao Chakwera na Chilima walipinga matokeo ya uchaguzi huo wakisema makosa yaliofanyika yaliathiri zaidi ya kura milioni 1.4 kati ya kura milioni 5.1 zilizopigwa.

Wagombea watatu wanatafuta wadhifa huo lakini ushindani mkali ni kati ya rais Peter Mutharika na kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutangazwa siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.