Pata taarifa kuu
MALAWI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Raia wa Malawi wapiga kura kumchaguwa rais wao mpya

Wananchi wa Malawi wanapiga kura leo katika marudio ya Uchaguzi wa urais, katika Uchaguzi ambao unaelezwa na wachambuzi kama kipimo cha demokrasia katika taifa hilo.

Mpiga kura nchini Malawi Mei 21 2019
Mpiga kura nchini Malawi Mei 21 2019 mbctv.malawi
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama kufutilia mbali ushindi wa rais Peter Mutharika mwezi Februari baada ya kubainika kwa udanganyifu na kuagiza uchaguzi mpya.

Rais Mutharika anatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera, huku kila mmoja akisema ana uhakika wa kushinda.

Mahakama mwezi Februari ilisema ushindi wa rais Peter Mutharika uligubikwa na udanganyifu mkubwa.

Mahakama ya Katiba ilichukuwa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo kutokana na dosari nyingi zilizoufanya uchaguzi huo usiwe huru, haki na wa kuaminika, alisema Jaji kiongozi wa Mahakama ya Katiba, Healey Potani.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019, Tume ya uchaguzi ilimtangaza Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 38.6 ya kura zote.

Uchaguzi unafanyika chini ya sheria mpya, ambapo mshindi sasa atahitaji kupata wingi wa kura wa 51% .

Kwa miezi kadhaa sasa, raia wa Malawi wamekuwa katika mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo. Ni zaidi ya mwaka sasa tangu mamilioni ya raia walipojitokeza katika uchaguzi wa bunge na urais.

Kumekuwa na maandamano ya kupinga serikali pamoja na kutokea kwa ghasia ambako kumetishia nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.