Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-USALAMA

Malawi yajiandalia uchaguzi wa urais Jumanne wiki hii

Raia wa Malawi wanatazamiwa kushiriki uchaguzi wa urais  kesho baada ya mahakama ya kikatiba nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019, Tume ya uchaguzi ilimtangaza Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 38.6 ya kura zote.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019, Tume ya uchaguzi ilimtangaza Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 38.6 ya kura zote. AMOS GUMULIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama mwezi Februari ilisema ushindi wa rais Peter Mutharika uligubikwa na udanganyifu mkubwa.

Mahakama ya Katiba ilichukuwa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo kutokana na dosari nyingi zilizoufanya uchaguzi huo usiwe huru, haki na wa kuaminika, alisema Jaji kiongozi wa Mahakama ya Katiba, Healey Potani.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019, Tume ya uchaguzi ilimtangaza Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 38.6 ya kura zote.

Matokeo hayo kwa majuma kadhaa yalisababisha maandamano makubwa ya wafuasi wa upinzani, huku serikali ikilaumiwa pakubwa kwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji.

Tume ya haki za binadamu nchini Malawi wakati huo ilisema mwezi Oktoba pekee wakati wa maandamano ya wafuasi wa upinzani, polisi na wanajeshi walitekeleza vitendo vya ukatili kwa kuwabaka wanawake hata mbele ya familia zao.

Kuna wagombea watatu watakaomenyana kwenye kinyang'anyiro hicho lakini ushindani mkubwa unatazamiwa kuwepo kati ya rais Peter Mutharika na mpinzani wake mkuu Lazarus Chakwera.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.