Mgomo wazorotesha shughuli katika hospitali za umma Malawi
Mgomo wa wauguzi wa kitaifa nchini Malawi umekwamisha shughuli katika hospitali za umma wakati huu nchi hiyo ikipambana na ugonjwa wa Covid-19.
Imechapishwa:
Wauguzi hao wanalalamikia mazingara magumu ya kufanyia kazi na kukosa vifaa vya kujilinda.
Wauguzi nchini Malawi wamegoma kulalamikia hatua ya serikali kushindwa kuwaajiri wauguzi zaidi na kuwapa vifaa vya kujilinda wakati huu wa janga la Corona.
Serikali ilikuwa imeahidi kuwaajiri maafisa 2000 wa afya ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Visa 17 vya Corona vimethibitishwa nchini Malawi, huku raia wakihofia kuwa huenda idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona ikaongezeka kutokana na hali ngumu inayowakabili wananchi wa taifa hilo.