Pata taarifa kuu

Kundi la GSIM lakiri kuhusika na mashambulizi ya Boulkessi na Mondoro

Kundi linalodai kutetea na kuunga mkono Uislam na Waislamu nchini Mali GSIM limekiri kuhusika na mashambulizi ya Septemba 30 katika miji ya Boulkessi na Mondoro katikati mwa nchi.

Kikosi cha jeshi la pamoja la G5 Sahel, kutoka Mali wakipiga doria karibu na mpaka na Burkina Faso, Novemba 2017.
Kikosi cha jeshi la pamoja la G5 Sahel, kutoka Mali wakipiga doria karibu na mpaka na Burkina Faso, Novemba 2017. © Daphné BENOIT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu usiku wiki hii kwenye mitandao ya kijamii, kundi la wanamgambo wa Kiislam, GSIM, linaloongozwa na Iyad Ag Ghali, lilidai kwamba zaidi ya askari 80 wa Mali waliuawa katika mashambulizi hayo.

GSIM ilingoja wiki moja kabla ya kudai kuhusika na mashambulizi hayo mawili katika kambi ya jeshi ya Mondoro na kambi ya kikosi cha ukanda cha G5 Sahel kutoka Mali katika mji wa Boulkessi.

Shambulio hili katika mji wa Boulkessi limekuwa tukio la hatari zaidi dhidi ya jeshi la Mali (Fama) tangu kutokea mapigano makali katika mkoa wa Kidal Mei 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.