Pata taarifa kuu
MALI-G5 SAHEL-USALAMA

Askari 25 wa Mali na wanajihadi 15 wauawa Boulkessi

Kulingana na taarifa rasmi, wanajeshi 25 wa Mali waliuawa katika mapigano Jumapili usiku, ambayo yameendelea Jumanne kati ya jeshi la Mali na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.

Jeshi la Mali likipiga doria Anderamboukane, katika Jimbo la Menaka, Machi 22, 2019.
Jeshi la Mali likipiga doria Anderamboukane, katika Jimbo la Menaka, Machi 22, 2019. © Agnes COUDURIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la watu wenye silaha walidhibiti kwa muda mfupi ngome za jeshi la Mali. Wanajeshi wengine 60 wa Mali hawajulikani waliko.

Bado haijafahamika idadi rasmi ya watu waliouawa katika mapigano hayo makali ya siku mbili yaliyotokea katika mji wa Boulkessi. Kwa sasa, serikali ya Mali ndiyo pekee inayotoa taarifa rasmi.

Kwa mujibu wa msemaji wa kikosi cha wanajeshi kutoka Mali, kilio chini ya usimamizi wa jeshi la pamoja la G5 Sahel, kikosi hicho kimepoteza askari 25, kulingana na ripoti ya awali. Askari wengine 60 wa Mali hawajulikani waliko kwa wakati huu, na jeshi limepata hasara kubwa kwa upande wa vifaa.

Zaidi ya wanajihadi 15 wameuawa katika mapigano hayo, kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano Yaya Sangare, na kuongeza kuwa jeshi la Mali lilifanikiwa siku ya Jumanne kurejesha kwenye himaya yake ngome zake.

Amethibitisha kwamba washambuliaji walidhibiti kwa saa kadhaa ngome za kikosi cha jeshi la G5 Sahel kutoka Mali. Lakini katika hali ya kukabiliana na adui, washirika wa Mali katika uwanja wa vita, nikimaanisha kikosi cha jeshi la Ufaransa cha Barkhane na kikosi cha Umoja wa Mataifa, waliingilia kijeshi Boulkessi na kuokoa jahazi, amesema Waziri Yaya Sangare.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.