Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Saba wauawa wakati wa maandamano makubwa Sudan

Hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini Sudan, huku jeshi likiendelea kushinikizwa kukabidhi madaraka kwa raia. Watu saba wameuawa Jumapili katika makabiliano kati ya jeshi na waandamanaji.

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji wakimiminika mitaani jijini Kahartoum, Jumapili mchana Juni 30, 2019.
Mamia kwa maelfu ya waandamanaji wakimiminika mitaani jijini Kahartoum, Jumapili mchana Juni 30, 2019. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika makabiliano hayo. Maelfu ya watu waliandamana kote nchini wakiomba jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Katika mji mkuu Khartoum, umati wa waandamanaji waliweza kufika kwenye ikulu ya rais, ambapo ni makao makuu ya Baraza la Jeshi la Mpito (TMC). Jata hivyo jeshi lilitumia mabamu ya machozi kwa kuwatawanya waandamanaji. Mamia ya askari wa akiba kutoka kikosi cha Usaidizi wa Haraka (FSR) walitumwa katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu Khartoum.

"Ujumbe wa askari hao ilikuwa kulinda waandamanaji, lakini hatukuamini watu walioshirikiana na waandamanaji. kulikuepo na watu kadhaa wenye silaha ambao waliwafyatulia risasi askari watatu wa kikosi cha Usaidi wa Haraka (FSR) na raia watano au sita, "amesema Mohamed Hamdane Daglo, Makamu wa rais wa Baraza la Jeshi la Mpito (TMC).

Haya yamejiri wakati huu Jumuiya ya Kimataifa ikitoa wito kwa jeshi kuacha kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji kama ilivyotokea mapema mwezi huu.

Viongozi wa waandamanaji, walikuwa wamaitisha maandamano ya watu Milioni moja hivi leo, lakini kwa sababu ya kukakatwa kwa huduma ya Internet, imekuwa ni vigumu, waandamanaji kukusanyika kama hapo awali.

Licha ya waandamanaji kupiga kambi katika Wilaya ya Bari na Mamura na Arkweit, Mashariki mwa jiji la Khartoum, walifukuzwa na maafisa wa polisi.

Maandamano haya yamekuja, wakati huu Umoja wa Afrika na Ethiopia kwa pamoja zikiwasilisha mikataba ya kuunda serikali ya mpito kati ya wanajeshi na waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.