Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-SIASA

Maandamano yaanza tena nchini Sudan, polisi watumia mabomu ya machozi

Polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji waliojitokeza jijini Khartoum nchini Sudan, kulishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia, huku waandamanaji wakiapa kwenda kupiga kambi nje ya Ikulu ya rais.

Waandamanaji nchini Sudan Juni 30 2019
Waandamanaji nchini Sudan Juni 30 2019 REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Haya yamejiri wakati huu Jumuiya ya Kimataifa ikitoa wito kwa jeshi kuacha kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji kama ilivyotokea mapema mwezi huu.

Viongozi wa waandamanaji, walikuwa wamaitisha maandamano ya watu Milioni moja hivi leo, lakini kwa sababu ya kukakatwa kwa huduma ya Internet, imekuwa ni vigumu, waandamanaji kukusanyika kama hapo awali.

Licha ya waandamanaji kupiga kambi katika Wilaya ya Bari na Mamura na Arkweit, Mashariki mwa jiji la Khartoum, walifukuzwa na maafisa wa polisi.

Maandamano haya yamekuja, wakati huu Umoja wa Afrika na Ethiopia kwa pamoja zikiwasilisha mikataba ya kuunda serikali ya mpito kati ya wanajeshi na waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.